Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chuo Cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA)

Taarifa kwa Umma kuhusu kufunguliwa kwa Dirisha la Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2024/202
31 May, 2024
Taarifa kwa Umma kuhusu kufunguliwa kwa Dirisha la Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2024/202

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA KUJIUNGA NA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO

2024/2025

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na NACTVET umefunguliwa rasmi leo tarehe 27 Mei, 2024.

Maombi ya udahili kwa kozi ambazo sio za Afya na Sayansi Shirikishi, na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika vyuo vilivyoko Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia tarehe 27 Mei hadi tarehe 14 Julai, 2024 kwa awamu ya kwanza.

Aidha, maombi ya kozi za Afya na Sayansi Shirikishi - Tanzania Bara, yatafanyika kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kuanzia tarehe 27 Mei hadi tarehe 30 Juni, 2024 kwa awamu ya kwanza.

Baraza pia linautaarifu umma kuwa kozi zinazoombwa na vyuo vinavyotoa kozi hizo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025 (Admission Guidebook for 2024/2025 Academic Year). Mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz).

Baraza linawasisitiza waombaji wote waandike taarifa zao kwa usahihi na umakini; na kutunza kumbukumbu watakazopatiwa na Baraza bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi/vyuo mbalimbali.

 

IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

TAREHE 27 Mei, 2024